Millionaire  Ads

Monday, November 7, 2016

Kijana na Ajira

Tags

Habari za Muda kijana mwenzangu najua tunakabiliwa sana na changamoto za ajira na mara nyingi kama kijana uwa tunapenda sana kazi za kuajiriwa kitu ambacho kwa sasa ni adimu kutokana na wingi wa vijana wanaotafuta ajira nchini na wengi Wao wana kiwango cha juu cha elimu kushinda wewe na wana chaneli kushinda wewe, Kijana mwenzangu suala la kuajiriwa kwa sasa ebu weka pembeni tupeana mawazo Jinsi ya kutengeneza pesa bila kuwepo na mtu atakayeweka sahihi kwenye hundi yako namaanisha kuwa na mwajiri. Kwa leo ngoja nikupe wazo moja naamini ukilifanyia kazi kijana hautabaki kama ulivyo, wazo hilo ni (kutengeneza chapati na maharage)
Tafuta eneo lenye shughuli nyingi za watu haswa stendi au sehemu zenye msongamano wa Biashara kwa mjini sehemu Hizo zipo nyingi ongea na uongozi wa pale wakupe eneo la kuweka meza yako na jiko mita mbili au tatu inatosha Kabisa.
Nunua vifaa vyako vya kutengenezea chapati meza na jiko pamoja na vyombo vichache vya kuanzia kisha Nunua mahitaji yako kama vile Unga wa ngano, maharage, mkaa na mafuta kisha anza kazi yako taratibu siku za kwanza haitakuwa rahisi ila kila uanapoendelea utaona manufaa jaribu kukadiria chapati zako ziwe tofauti na hizo anazopika watu wengine na ubora uwe mzuri utakuwa unauza angalau chapati 2 na maharage bakuli 1 shilingi 1000 anza Biashara yako asubuhi mpaka usiku utapata wateja wengi kiasi cha kwamba unahitaji kuajiri mtu mwingine akusaidie wazoeshe wateja wako wakija huduma zipo kila wakati utapata wateja wengi sana kwani kama ni wa piga debe wote na madereva wanahitaji huduma ya haraka wataipata kwako na mwisho wa siku unaweza tengeneza brand yako na ukawa boss mkubwa kwa kutengeneza chapati kadri siku zinavyokwenda kuwa mbunifu wawekee maziwa juice nk nakuambia kijana mwenzangu utahitaji kuajiriwa tena haijalishi una kiwango gani cha elimu.

Imetayarishwa na John Nnko

On Nov 8, 2016 9:42 AM, "razak Mbena" <chatguestforum@gmail.com> wrote:
Samahani kuna makosa kidogo kwenye email maalumu hapo juu tafadhali tumia hii hapa chini 

onlinelibrarytz.ajira@blogger.com

2016-11-07 22:37 GMT-08:00 razak Mbena <chatguestforum@gmail.com>:
Hongera kwa kuchaguliwa kuwa mwandishi wa blog. Tunakupa blog ya www.ajirazilizotangazwa.blogspot.com

Mara upatapo ujumbe huu anza kuandika makala zako unazozipenda. Usipoandika chochote ndani ya siku tatu blog hii atapewa mwingine anayeihitaji. Tumepokea maombi zaidi ya elfu tatu hivyo wapo watu ambao wanahitaji kazi hii nzuri ya kufanya muda wa ziada yaani ukiwa unapumzika.

Malipo: Utalipwa kwa idadi ya watu wanaotazama blog yako. Kiasi cha chini kutumiwa pesa ni utakapofikisha shilingi laki moja. Hakuna kikomo cha malipo hata wakitazama watu milioni moja kwa mwezi utalipwa pesa yako yote.

Faida nyingine za kuwa mwandishi wetu ni kwamba pesa zote za matangazo unayopokea kutoka kwa watembeleaji wako na kutupa sisi tukuwekee tangazo hilo kwenye blog ni zako, yaani ukipata mteja anataka umtangazie biashara yake kwenye blog yako kubaliana bei ya tangazo kwa mwezi na hakikisha amekulipa pesa zote kisha tupe tangazo tuliweke kwenye blog. 

Kuna faida nyingine nyingi tutaendelea kukujulisha kadili unavyozidi kuandika makala zako au habari na kuitangaza blog yako facebook mtaani kwako kwa marafiki zako ili upate watu wengi wanaoitembelea na upate pesa nyingi kila mwezi.

Usihofu tutakufundisha mbinu nyingi za kupata watembeleaji si chini ya elfu kumi kwa siku ili angalau kila mwezi ulipwe shilingi laki tatu na pesa zaidi za matangazo utakazozipata kama tulivyoeleza hapo juu.

Jinsi ya kuanza kuandika makala kwenye blog yako. Ukiwa kwenye email yako nenda sehemu ya kuandikia ujumbe au email kisha andika makala yako au habari kisha itume kwenda kwenye anwani maalumu ya blog yako ambayo ni 


Hapo hapo makala yako itaenda kwenye blog yako.

ZINGATIA: Hakikisha mwisho wa makala au habari yako unaandika jina lako Mfano "imetayarishwa na Anna Tesha"

Tunakutakia kazi njema.

2016-10-30 10:11 GMT-08:00 John Nnko <nnkojuniour@gmail.com>:

Habari nimeona ujumbe toka chatguest na vitu nitakavyopendelea kuandika ni Kuhusu
1 vijana na ajira
2 Nakupenda mazingira
3 Malezi ya Watoto kwa taifa bora



Wednesday, October 19, 2016

Ajira zilizotangazwa ni mtandao unaokuwezesha kijana kupata kazi kwa haraka

Tags
Ajira zilizotangazwa ni mtandao wako kijana unaetafuta kazi. Utapata habari zote zinazohusiana na ajira kazi zinazotangazwa utumishi kazi zinazotangazwa kwenye makampuni kazi zinazotangazwa kwenye mashirika binafsi na ajira zote kama ajira za walimu ajira JKT na kwingineno.

Una kampuni unataka wafanyakazi wenye ujuzi andika tangazo lako la kazi tuma kwenda kwenye email hii maalumu onlinelibrarytz.ajira@blogger.com Tangazo lako litakuja hapa moja kwa moja huduma hii ni bure hulipii chochote. Mtandao huu unatembelewa  na vijana zaidi ya elfu kumi kwa siku hivyo utapata wafanyakazi wenye ujuzi na taaluma unayotaka.

Nawe kijana unayetafuta kazi usisubiri mpaka uone tangazo ndio utume maombe tumia mtandao huu kujitangaza kile ulichosomea. andika ujumbe ukielezea umesoma kozi gani na unatafuta kazi gani kisha tuma kwenda kwenye email ya onlinelibrarytz.ajira@blogger.com ili wanaohitaji wafanyakazi wawasiliane na wewe moja kwa moja.

Tumia fulsa pata ajira Tumia fulsa pata wafanyakazi wenye ujuzi